Skip to main content

Chuja:

Siraj Kalyango

Sudan Kusini ni hatari kwa watoa misaada-UNICEF

Hali ya sasa ya kiusalama nchini Sudan Kusini si shwari kwa wafanyakazi wanaotoa misaada.

Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF, Henrietta H. Fore amesema hayo leo akieleza kuwa shirika lake pamoja na mengine ya misaada nchini Sudan Kusini yanafanya kazi katika mazingira hatari wakati wakitoa misaada muhimu inayohitajika kwa watoto pamoja  na vijana.