Taka za kielektroniki zasalia kwenye makabati majumbani- Ripoti

Takwimu za kiwango cha taka za kielektroniki zilivyotupwa mwaka jana. Vifaa vidogo ni pamoja na plagi za umeme huku vifaa vidogo vya teknolojia vikiwa ni pamoja na simu za kiganjani. (Picha: Global e-waste monitor report)

Taka za kielektroniki zasalia kwenye makabati majumbani- Ripoti

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa imebaini ongezeko kubwa la taka za kielektroniki ulimwenguni.

Taka hizo ni pamoja na betri chakavu, plagi za umeme, majokofu, simu za kiganjani na kompyuta ambazo kiwango chake mwaka 2016 kilifikia tani za ujazo milioni 44.7.

Kiwango hicho ni ongezeko kwa asilimia 8 ikilinganishwa na mwaka jana na mwelekeo ni ongezeko zaidi kutokana na sababu mbalimbali ikiwemo kuporomoka kwa bei za vifaa vya kielektroniki na umeme na hivyo kuwa kishawishi kwa watu kununua vifaa vipya na kutupa hovyo vya zamani.

Ripoti hiyo inasema kuwa ujazo wa taka za mwaka jana unaweza kujaa kwenye malori milioni 1.23 ya tani 40 na kupanga msururu kuanzia New York Marekani hadi Bangkok Thailand na kurejea.

Ruediger Kuehr ambaye ni mmoja wa waandishi wa ripoti hiyo na anasema kilichomstaajabisha kwenye ongezeko hilo la taka ni kwamba

(Sauti ya Ruediger Kuehr)

“Licha ya ukweli kwamba zaidi ya asilimia 60 ya wakazi wa dunia wako kwenye maeneo ambako kuna mifumo ya kudhibiti taka za kielektroniki pamoja na sheria na sera, bado usimamizi hakuna.”

image
Baadhi ya taka za kielektroniki zikiwemo kompyuta na vifaa vingine vya kielektroniki ambapo ripoti inasema vingine vikishachakaa husalia kwenye makabati majumbani bila utupaji sahihi. (Picha:UNEP)
Anasema cha kusikitisha zaidi takwimu hazipatikani, mathalani barani Afrika hivyo anasema..

(Sauti ya Ruediger Kuehr)

“Hatuna takwimu na takwimu ni muhimu kwa watunga sera, wamiliki wa viwanda na wengineo kwa ajili ya kuweka mipango na kujenga miundombinu.”

Ripoti hiyo iliandaliwa kwa pamoja ni jitihada za pamoja za chuo kikuu cha Umoja wa Mataifa, UNU, shirika la mawasiliano la Umoja wa Mataifa , ITU na chama cha kimataifa cha taka ngumu,