Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji ya kimbari asilani yasiwe na nafasi sasa hata milele:UN

Mauaji ya kimbari asilani yasiwe na nafasi sasa hata milele:UN

Katika kuwaenzi wahanga wa mauaji ya kimbari, ofisi ya Umoja wa mataifa inayoratibu juhudi za kuzuia mauaji hayo imezindua ombi kwa nchi wanachama la kuridhia mkataba wa 1948 wa kuzuia mauaji ya kimbari ifikapo mwisho wa mwaka 2018 kama bado hawajafanya hivyo.

Katika ujumbe wake wa kuadhimisha siku hii ya kuwakumbuka na kuwaenzi wahanga wa mauaji ya kimbari ambayo kila mwaka huwa kila mwaka Desemba 9, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema mauaji ya kimbari hayatokei kwa bahati mbaya, ni ya makusudi, yakiwa na watangulizi na ishara zote za onyo.

Ameongeza kuwa mara nyingi mauaji hayo yanatokana na miaka mingi ya kutengwa, kunyimwa haki za binadamu na makossa mengine, na kwa sababu mauaji ya kimbari yanaweza kutokea wakati wowote, wa vita na wa amani amesisitiza ni lazima kila mtu kuwa makini.

Guuterres amesema licha ya maana ya mauaji ya kimbari kuainishwa bayana kwenye mkataba pamoja na kuelewa hatari zake , bado mauaji hayo yameendelea kutokea mara kadhaa.

Amesisitia kuwa bado watu tuanachukua hatua baada ya tukio kutokea badala ya kulizuia , na hivyo hatua hizo zinakuwa zimechelewa, amehimiza ni lazima kuongeza juhudi sasa kuchukua hatua mapema na kuzuia migogoro kkabla haijafika hatua mbaya.

image
Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusukuzuia mauaji ya kimbari , Adama Dieng akizungumza katika maadhimisho ya kuwakumbuka wahanga wa mauaji ya kimbari kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York. Picha na UN/Manuel Elias
Naye mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari Adama Dieng amesema mauaji ya kimbari hayapaswi kuwa sehemu ya maisha yetu ya sasa au ya baadaye. Sio ajali na sio kitu ambacho hakiepukiki, ni uzembe wetu wa kutochukua hatua au kutowajibika kushughulikia ishara zote ambazo zinaruhusu mauaji hayo kutekelezwa.

Ameongeza kuwa uhalifu wa mauaji ya kimbali haukuanza na mkataba wa kuzuia mauaji hayo na kwa bahati mbaya haukuisha na mkataba huo.

Hadi kufikia leo jumla ya nchi 149 ikiwemo moja ambayo sio mwanachama wa Umoja wa Mataifa wameridhia mkataba huo , na sasa wito ni kwa nchi 45 zilizosalia kufanya hivyo ifikapo mwishoni mwa mwaka 2018.