Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kuwezesha mwanamke bila kuelimisha mwanaume ni bure- UNWomen

Mary Mtaki pamoja na mama yake dukani lao jijini Tunduma, Tanzania. Picha: UN Women Tanzania Tanzania / Deepika Nath

Kuwezesha mwanamke bila kuelimisha mwanaume ni bure- UNWomen

Siku 16 za kupinga ukatili dhidi ya wanawake zikiendelea kupigiwa chepuo kila kona ulimwenguni, imeelezwa kuwa kumwezesha mwanamke bila kumuelimisha mwanaume hakuna tija yoyote. Selina Jerobon na maelezo zaidi.

(Taarifa ya Selina Jerobon)

Mehjabeen Alarakhia ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya kuwezesha wanawake kiuchumi katika shirika la masuala ya wanawake la Umoja wa Mataifa, UNWomen nchini Tanzania, akihojiwa na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha umoja huo jijini Dar es salaam.

Bi. Alarakhia amesema ingawa umaskini katika familia nao huongeza mizozano kati ya mume na mke lakini pia…

(Sauti ya Mehjabeen Alarakhia)

Afisa huyo wa UNWomen nchini Tanzania akaelezea pia madhara ya ukatili wa kipigo kwa mwanamke majumbani…

(Sauti ya Mehjabeen Alarakhia)