Taka za kielektroniki bado tatizo- Ripoti

5 Disemba 2017

Uchafuzi wa mazingira utokanao na utupaji hovyo wa taka za kielektroniki na umeme umesababisha Umoja wa Mataifa kuweka msisitizo wa udhibiti wa utupaji wa taka hizo.

Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa leo inasema hatua hiyo inatokana na ukweli kuwa matumizi ya vifaa vya kieletroniki kama vile kompyuta na vile vya umeme kama vile majokufu yanazidi kuongezeka kila uchao.

Ripoti imebaini kuwa pindi matumizi ya vifaa hivyo yanapomalizika husafirishwa hadi nchi zinazoendelea kwa matumizi zaidi huku uchakataji wake ukitishia afya za wafanyakazi.

Imeelezwa kuwa kitendo hicho ni kinyume na lengo namba 3 la malengo ya maendeleo ya milenia, SDG kipengele cha 9 ambacho kinataka hatua zaidi kuepusha magonjwa na vifo vitokanavyo na uvutaji wa hewa chafu.

Kwa mantiki hiyo ripoti imetaka mfumo wa Umoja wa Mataifa kuchukua hatua katika uratibu wa sera ili kuratibu utupaji sahihi wa taka za kielektroniki.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa UNGA76 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter