Shule ya Michungwani, Handeni Tanga yapata jibu la utoro kwa wanafunzi

30 Novemba 2017

Lengo namba 4 la malengo endelevu ya Umoja wa Mataifa, SDGs, linapigia chepuo elimu bora. Hii inamaanisha pamoja na mambo mengine watoto siyo tu waandikishwe shule bali pia wamalize masomo yao hadi mwisho bila kukosa.

Hata hivyo utoro unaonekana kuwa ni kikwazo katika baadhi ya nchi na Tanzania ni miongoni mwao. Hata hivyo kwa kutambua changamoto hiyo tayari serikali imeanza kuchukua hatua, mathalani huko wilaya ya Handeni mkoani Tanga, shule ya msingi Michungwani yenye jumla ya wanafunzi 1285.

Utoro kwa muda mrefu ulikuwa ni tatizo lakini sasa muarobaini umepatikana. Je nini kimefanyika? Martin Mhina wa radio washirika Voice of Africa kutoka Korogwa, Tanga ametembelea shule hiyo kusaka jibu.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter