Nuru yaangukia wahamiaji walioteswa Libya
Shirika la Umoja wa Mataifa la uhamiaji IOM, limeanza operesheni ya kuwarejesha makwao maelfu ya wahamiaji, kufuatia makubaliano baina ya shirika hilo, Muungano wa Afrika, AU, Muungano wa Ulaya, EU na serikali ya Libya.
Hatua hii ni baada ya ripoti za vitendo vya kikatili dhidi ya wahamiaji hao ikiwemo unyanyasaji, utumikishaji na kuuzwa utumwani.
Wahamiaji hao walisafirishwa kwa ndege zilizokodishwa na IOM ambapo miongoni mwa ndege hizo ilitua Conakry, Guinea ikiwa na wahamiaji 155, ambapo 10 kati yao ni watoto.
IOM inalenga kusafirisha jumla ya wahamilaji 15,000 kutoka vituo vya mbalimbali Libya huku ikiendeleza jitihada za kuwatafutia wengine makazi ya kudumu kwenye nchi ya tatu.