Ufugaji nyuki sasa ni mtaji dhidi ya umaskini huko Kyela, Tanzania
Kupitia lengo namba moja la kutokomeza umasikini lililomo kwenye ajenda ya maendeleo endelevu ya Umoja wa Mataifa ya mwaka 2030, serikali zinahimizwa kutafuta mbinu mbadala kuwawezesha wananchi kupitia miradi mbalimbali ili kujikwamua na umasikini ifikikapo mwaka 2030.
Tanzania ni nchini mojawapo ambako serikali imechukua jukumu la kutoa elimu ya SDGs kwa kutafsiri malengo yao endelevu kwa lugha ya kiswahili ili kutoa mwongozo kwa wananchi na pili kuwapatia fursa za ujasiriamali kupitia miradi mbalimbali kama ufugaji, uvuvi, kilimo na kadhalika.
Lakini zaidi ya yote kuna ufugaji nyuki, ambapo Alex Punte wa redio washirika ya Kyela FM kutoka Mbeya mkoani Tanzania amefuatilia ufugaji nyuki katika wilaya ya Kyela nchini Tanzania.