Marufuku ya "viroba" Tanzania yaleta nuru kwa vijana
Katika ajenda ya Umoja wa Mataifa ya malengo ya maendeleo endelevu SDGs au ajenda 2030, vijana kama nguvu kazi na mustakabali wa dunia wanapewa jukumu la kijiendeleza ili kujikwamua na suala la umasikini siku za usoni.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres katika hutuba yake huko Abidjan, Cote D’Ivoire amezieleza serikali za Afrika na zile za Ulaya kwamba ili kufikia mustakhbali bora ni lazima kuwekeza katika vijana leo.
Katika kufanikisha hilo, Alex Punte wa radio washirika, Kyela FM huko Mbeya nchini Tanzania anatupeleka Kyela mjini ambako kuna nuru sasa kwa vijana baada ya serikali ya Tanzania kupiga marufuku matumizi ya pombe zilizokuwa zinauzwa kwenye vifungashio vya vifuko, maarufu kama viroba, ambayo ilikuwa inaathiri sana vijana na hivyo kuhatarisha mustakhbali wao.