Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Panua wigo wa bidhaa ili kufanikisha SDGs- Ripoti

Picha: FAO
Sri Lanka kununua mchele kutoka Bangladesh.

Panua wigo wa bidhaa ili kufanikisha SDGs- Ripoti

Umoja wa Mataifa umesemanchi zinazoendelea ambazo ni tegemezi kwa bidhaa ni lazima ziwe na mpango wa kupanua wigo wa bidhaa zao ili kuweza kufanikisha ajenda 2030 ya maendeleo endelevu, SDGs.

Mashirika hayo lile la chakula na kilimo, FAO na kamati ya maendeleo ya biashara, UNCTAD wamesema hayo katika ripoti yao ya leo.

Wamesema ni lazima kufanya marekebisho ya kisera kwa kuzingatia kuwa bei za bidhaa za vyakula na vile zisizo za vyakula zitasalia za chini kando mwa bei ya mafuta.

Kwa mantiki hiyo ripoti inataka bidhaa kuongezewa thamani ili hata bei za mazao zinaposhuka bado wakulima wawe na chanzo kingine cha mapato.

Maeneo yaliyohusishwa na ripoti hiyo ni pamoja na uzalishaji wa soya Argentina na Brazil, mpunga huko Bangladesh, uchimbaji wa almasi huko Botswana na Sierra Leone pamoja na kilimo cha pamba Burkina Faso na buni na ndizi nchini Costa Rica.

Ripoti hiyo ya UNCTAD na FAO inasema iwapo será jumuishi zitaandaliwa kwa kipindi cha miaka 15 ijayo, itapanua wigo wa shughuli za kiuchumi na kuunganisha sekta ya bidhaa na uchumi wa taifa.