Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Asasi za kiraia zinaweza kuchangia vita dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu: Nelly

Usafirishaji haramu wa binadamu. Picha: UNICEF

Asasi za kiraia zinaweza kuchangia vita dhidi ya usafirishaji haramu wa binadamu: Nelly

Wakati Umoja wa mataifa na mashirika yake yanayohusika na masuala ya wakimbizi na wahamiaji wakiendelea kukusanya taarifa kuhusu ripoti za usafirishaji haramu wa binadamu na biashara ya utumwa dhidi ya wahamiaji nchini Libya, wanaharakati kutoka asasi za kiraia wanasema asasi hizo zikiwezeshwa zinaweza kuchangia katika vita hivyo. Leah Mushi na taarifa kamili

(LEAH NA TAARIFA KAMILI)

Kauli hiyo imetolewa na Nelly Niyonzima mwanaharakati kutoka asasi za kiraia ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi inayojihusisha na kuwakwamua wanawake na watoto katika masuala ya unyanyasaji, ijulikanayo kama Connected hearts.

Akizungumza  na idhaa hii, Bi Niyonzima amesema licha ya kuonekana kuwa bado biashara hiyo inashamiri hasa baada ya taarifa za hivi karibuni za kuwepo kwa biashara ya utumwa nchini Libya ambayo chimbuko lake ni usafirishaji haramu wa binadamu, hatua zinazopaswa kuchukuliwa ni.

( Sauti Nelly)

Kuhusu jumuiya ya kimataifa amesema.

( Sauti Nelly)

Mapema juma hili, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amelaani hatua ya biashara ya utumwa nchini Libya  na kutaka vyombo vya sheria kuchukua hatua dhidi ya vitendo hivyo.