UM wapongeza hatua ya kuruhusu ndege za misaada kuingia Yemeni
Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu na masuala ya dharura OCHA limefurahishwa na taarifa ya ujumbe wake huko Riyad Falme za kiarabu kwamba ndege ya abiria ya shirika hilo UNHAS imeruhusiwa kuanza safari zake kutoka Amman kwenda Sana’a nchini Yemen kuanzia kesho Jumamosi.
Kwa mujibu wa Jens Laerke msemaji wa OCHA japo hawajapata ufafanuzi kuhusu kupata ruhusa za safari kutoka bandari ya Hudayday na Saleef kwajili ya kusafirisha mahitaji ya kibunadamu, amefurahishwa na zoezi hilo la awali na kwamba UM unategemea kupata ruhusa ya ndege zigine kutoka DJibouti kuelekea Sana’a.
(Sauti ya Jens Laerke )
“Kama Mashirika ya kibinadamu tunatoa misaada kwa watu milioni 7 Yemen ambao kimsingi wanatutegema kwa kila kitu. Kwa mfano tunasambaza maji kwa takribani watu milioni 4 wakati huu wa jaa kali nchini humo.”
Aidha Jens amesema zoezi la kupeleka misaada pia litasaidia kutokomeza ugonjwa wa kipindupindu ambao umekua tishio kwa watu wengi nchini Yemeni kutokana na kukosa huduma ya maji safi.