Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya homa ya ini bado ni safari ndefu-WHO

Vita dhidi ya homa ya ini bado ni safari ndefu-WHO

Takwimu kutoka nchi 28 zinazobeba takriban asilimia 70 ya mzigo wa ugonjwa wa homa ya ini au Hepataitis zinaonyesha hatua zimepigwa katika kutokomeza ugonjwa huo.

Hiyo ni kwa mujibu wa ripoti ya Shirika la afya Ulimwenguni, WHO katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa homa ya ini duniani mwaka huu kauli mbiu ikiwa “Tokemeza homa ya ini” kwa ajili ya kuchagiza juhudi kufikia malengo ya maendeleo endelevu, siku hiyo huadhimishwa kila mwaka Julai 28. Takwimu zinaonyesha kwamba nchi zenye mzigo mkubwa wa gonjwa hilo zimeweka mikakati na malengo na zaidi ya nusu zimewekeza fedha katika kukabiliana na ugonjwa huo.

WHO ambayo wiki hii imezindua tiba mbadala ya kukabiliana na homa ya ini aina ya C kwa ajili ya kuimarisha upatikanaji wa matibabu na chanjo ya kuzuia kuenea kwa homa ya ini aina B na C pia inatoa wito kwa nchi kuendeleza juhudi zao ili kutokomeza ugonjwa huo unaosababisha vifo.

Akizindua ripoti hiyo Mkurugenzi wa WHO kitengo cha HIV na programu ya homa ya ini Dr Gottfried Hirnschall amesema mtu mmoja kati ya kumi wanafahamu wanaugua homa ya ini na kwamba wanaweza kusaka matibabu akiongeza kuwa hilo halikubaliki, hatahivyo amesema

(DR GOTTIFRIED CUT)

“Ninataka kuwa mwenye matumaini na nadhani tuna sababu ya kuwa na matumaini, baadhi ya nchi zimeimarsiha juhudi, zingine bado zinaangalia upande mwingine, zingine zinajiandaa kwa kiasi kwa kuweka mikakati.”

Homa ya ini inayoambukiza iliathiri watu milioni 325 kote ulimwenguni mwaka 2015 huku watu milioni 257 wakiishi na homa ya ini aina ya B na wengine milioni 71 aina ya C- aina mbili kati ya tano zinazosababisha idadi kubwa zaidi ya vifo. Mwaka 2015 homa ya ini ilikatili maisha ya watu milioni 1.34 duniani.

Akizindua ripoti hiyo Mkurugenzi wa WHO kitengo cha HIV na programu ya homa ya ini Dr Gottfried Hirnschall amesema mtu mmoja kati ya kumi wanafahamu wanaugua homa ya ini na kwamba wanaweza kusaka matibabu akiongeza kuwa hilo halikubaliki, hatahivyo amesema