Uchaguzi wa sera muhimu kuboresha ajira ya wahamiaji-ILO

28 Juni 2017

Jumuiya ya kimataifa inapaswa kuimarisha utawala wa masuala ya uhamiaji na kupata njia mpya za kuboresha maisha na hali ya kazi ya wafanyakazi wahamiaji, amesema mkurugenzi mkuu wa shirika la kazi duniani ILO, Guy Ryder, akibainisha kuwa asilimia 74 ya wahamiaji wenye umri wa kufanya kazi wapatao milioni 150 wako katika soko la ajira na wanasaka kazi nzuri.

Ryder ameyasema hayo katika mkutano wa 10 wa jukwaa la kimataifa kuhusu uhamiaji na maeendeleo (GFMD) linalofanyika mjini Berlin nchini Ujerumani. Akijikita na kauli mbiu ya mkutano wa mwaka huu “kuelekea mkataba wa kijamii kwa ajili ya uhamiaji na maendeleo”, Ryder amehimiza fursa inayotokana na majadiliano kuhusu mikakati mipya ya kimataifa ya wahamiaji.

Pia amesisitiza umuhimu wa kuchukua hatua ambazo zitaleta mabadiliko ya kweli katika maisha ya wahamiaji wanaowasili pwani wakisaka usalama au mustakhbali bora.

Amesema endapo dunia itazingatiafaida za uhamiaji kwa pande zote husika, basi sera ni muhimu .

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter