Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya dola milioni 350 zaahidiwa kusaidia wakimbizi Uganda

Zaidi ya dola milioni 350 zaahidiwa kusaidia wakimbizi Uganda

Mkutano wa mshikamano na wakimbizi nchini Uganda umekunja jamvi hii leo kwa ahadi za dola milioni 350 za kuisaidia Uganda kukabiliana na dharura ya wimbi la wakimbizi.

Katika kipindi cha mwaka mmoja tu idadi ya wakimbizi nchini humo imeongezeka zaidi ya mara mbili kutoka laki tano na kufikia zaidi ya milioni 1.25.

Wengi wa watu hao wamekimbia vita na zahma ya kibinadamu nchini Sudan Kusini. Mwenyeji wa mkutano huo uliofanyika mji mkuu Kampala ni Rais wa Uganda Yoweri Museveni na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa , António Guterres.

Guterres amepongeza mkutano huo akisema umekuwa wa mafanikio

(SAUTI YA GUTERRES)

“Nadhani huu ni mwanzo mzuri lakini hatuwezi kuishia hapo. Tunahitaji kuendelea, na nchi nyingi zimesema hazikuweza kutoa ahadi leo , lakini zitatangaza ahadi zao katika wiki chache zijazo kiasi zaidi cha fedha. Nadhani tunaweza kumpongeza Rais wa Uganda kwa sababu mkakati huu kwa maoni yangu umefanikiwa.”