Ombi la msaada wa kibinadamu 2017 lafikia bilioni 23.5:UM

21 Juni 2017

Watu milioni 141 katika nchi 37 duniani wanahitaji msaada wa kibinadamu hivi leo na idadi hiyo inatarajiwa kuongeza umesema Umoja wa Mataifa Jumatano. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFA YA FLORA)

December mwaka 2016 Umoja wa mataifa na washirika wake walilizindua ombi la dola bilioni 22 za msaada wa kibinadamu kwa mwaka 2017 hadi sasa fedha zilizokusanywa ni bilioni 6.2 pekee.

Umoja wa mataifa unasema tangu mwaka jana kumekuwa na ongezeko la watu milioni nane wanaohitaji msaada kutokana na vita, njaa, na majanga na hivyo kuongeza kiasi cha fedha zinazohitajika hadi dola bilioni 23.5.

Fedha hizo ni za kuwasaidi watu zaidi ya miloni 100 katika nchi za Madagascar, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Kenya, Uganda, Msumbiji, Nigeria, Somalia, Sudan kusini na Yemen.

Jens Laerke ni msemaji wa shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA

(SAUTI YA JENS LAERKE)

Akizungumzia umuhimu wa usaidizi wa kibidamu Mkuu wa operesheni katika ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu misaada yakibinadamu OCHA John Ging anasema.

( Sauti Ging)

‘‘Ikiwa kuna yeyote anayetoa wito wa kuwezesha vita, kwa mtizamo wangu, kwanza lazima atoe wito wa kuongeza fedha za usaidizi wa kibinadamu, angalau katika kiwango ambacho kimeahidiwa na nchi zote wanachama katika makakati wa kuwezesha malengo ya maendeleoendelevu"

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter