Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamilioni Gaza wakwamuliwe, hali tete-Mladenov

Mamilioni Gaza wakwamuliwe, hali tete-Mladenov

Ukanda wa Gaza sasa ni vipandevipande na watu milioni mbili wanapaswa kukombolewa , amesema leo Mratibu Maalum wa Umoja wa Mataifa katika mchakato wa amani Mashariki ya kati Nickolay Mladenov.

Bwana Maldenov ameliambia baraza la usalama ambalo limekutana Jumanne kujadili hali katika ukanda huo, akisema ni muhimu viongozi wa Palestina na Israel kurejelea majadiliano kwa ajili ya suluhu ya nchi hizo mbili.

Amesema masuala yote ya kuhitimisha mwajadiliano yaweza kufikiwa kwa makubaliano ya pande zote, kwa mujibu wa sheria za kimataifa, na azimio la baraza la usalama namba 2234 la usitishaji wa ujenziwa makazi katika maeneo yanayokaliwa ya waPalestina ambalo amedai bado Israel haijalitimiza.

Mratibu huyo Maalum wa Umoja wa Mataifa katika mchakato wa amani Mashariki ya kati Mladenov, amelaani hatua ya mamlaka  Palestina kuendelea kuwahamasisha magaidi kama mashujaa. Ameonya kwamba.

(Sauti Mladenov)

‘‘Wapalestina milioni mbili walioko Gaza, hawawezi kuendelea kushikiliwa mateka watokanao na migawanyiko. Kuendelea kwa hili, huzalisha misimamo mikali. Tuna jukumu la pamoja la kuzuiia hili, tuna wajibu wa kuzuia janga la kibinadamu.’’