Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hali yazidi kuwa mbaya Kasai DRC-Zeid

Hali yazidi kuwa mbaya Kasai DRC-Zeid

Hali ya kibinadamu imezidi kuzorota katika majimbo ya Kasai nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC huku baadhi ya watu wakichochea chuki za kikabila na kusababisha hofu na mashambulizi ya kupangwa dhidi ya raia.

Hayo yamesemwa na Kamishina mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein Jumanne akiwasilisha taarifa kwenye kikao cha 35 cha baraza la haki za binadamu mjini Geneva Uswis, na kuongeza kuwa kuna taarifa mbaya za mauaji, yakijumuisha watoto wadogo wengine wana wakiwa na umri wa miaka miwili tu, katika mikoa ya Kasai, Kasai Kati, na Kasai Mashariki.

Zeid ameendelea kuhimiza kufanyika kwa uchunguizi wa kimataifa dhidi ya ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu na ukatili mwingine unaondelea nchini DRC ikiwemo mashambulizi ya raia, vituo vya afya na wahudumu wa afya katika vijiji 20 eneo la Kamonya ambako watu 90 waliuawa.