Tunafuatilia kwa karibu kinachoendelea Tunisia:UN
Ofisi ya haki za binadamu ya Umoja wa Mataifa leo imesema kuwa inafuatailia kwa karibu maanadamano yanayoendelea nchini Tunisia , athari zake na hatua zinazochukuliwa na serikali ya nchi hiyo. Siraj Kalyango ana maelezo zaidi.
(TAARIFA YA SIRAJI KALYANGO)
Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi ya hiyo,Rupert Colville, hofu yao ni kuhusu idadi kubwa ya watu wanaokamatwa katika maandamano hayo yamepelekea watu 778 kukamatwa tangu jumatatu,kati ya hao 200 ni wale wenye umri ulio kati ya 18 na 21.
Msemaji huyo ametoa mwito kwa wahusika nchini Tunisia kuhakikisha kuwa watu hawakamatwi kiholela na kwa wale wote wanaokamatwa wanaheshimiwa kwa haki zao zote kuheshimiwa Aidha amesema kuwa watawala nchini Tunisia lazima wahahakikishe kuwa yeyote yule anaetimiza haki yake ya kujieleza pamoja na uhuru wa kukusanyika hazuiliwi kufanya hivyo. Pia amesem akuwa wakati huu ikiwa inasubiriwa kuadhimisha mapinduzi ya mwaka 2011 yaani januari 14, ni jambo la umuhimu sana kuwa waandamanaji wanafanya hivyo kwa njia za amani.
Bwana Colville anatoa mwito.
(SAUTI YA RUPERT COLVILLE)
“ Tunaelewa kumetokea wizi wa ngawira, uharibifu wa mali pamoja na ghasia miwemo uharibifu wa vituo vya polisi na maduka. Tunawaombawaandamanaji kujizuia na kuwa watulivu. Wanaoandamana kwa amani hawapaswi kulaumiwa kuhusika na visa vya ghasia na kuweza kuaadhibiwa.”
Ofisi hiyo ya haki za binadamu pia imetoa wito wa to work together towards resolving, with full respect for human rights, the economic and social problems underpinning the unrest. The UN Human Rights Office in Tunisia will continue to closely monitor the situation.