Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

CAR lazima ichukue hatua sasa kulinda watu wake na haki:UM

CAR lazima ichukue hatua sasa kulinda watu wake na haki:UM

Jamhuri ya Afrika la Kati CAR inashuhudia hali isiyo "endelevu" inayochangiwa na kuenea kwa vikundi vyenye silaha na kuongezeka kwa ukiukwaji wa haki za binadamu, hivyo serikali inapaswa kuchukua hatua sasa kabla kitumbua hakijaingia mchanga ameonya , mtaalam wa Umoja wa Mataifa.

Marie-Thérèse Keita Bocoum, mtaalamu huru wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa nchini CAR amesema  vitendo vya ukatili wa makundi yenye silaha vinasambaa kwa kasi katika maeneo ya  Kusini na katikati mwa nchi hususan majimbo ya Ouaka, Mbomou na Basse-Kotto.

Amesema hali hiyo sio endelevu na kuitaka serikali kuchukua udhibiti wa mipaka yake bila kuchelewa ili kuhakikisha usalama na utawala wa sheria. Ameonya kwamba kutakuwa na athari kubwa hali hii ikiendelea, wahusika wa ukiukwaji wa haki za binadamu wakiachwa huru na uchunguzi kutofanyika.