Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki ya afya kwa wananchi bado inasiginwa- Baraza

Haki ya afya kwa wananchi bado inasiginwa- Baraza

Maeneo mbali mbali duniani hivi sasa haki ya msingi ya kupata huduma ya afya kwa binadamu bado inasalia ndoto.

Naibu Kamishna Mkuu wa haki za binadamu Kate Gilmore amesema hayo akihutubia kikao cha 35 cha Baraza la haki za binadamu huko Geneva, Uswisi hi leo ambacho kimeangazia haki ya msingi ya watu kupata huduma ya afya.

Amesema ingawa serikali zina wajibu wa kisheria kuwapatia wananchi huduma hiyo, bado kuna vikwazo.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa shirika la afya ulimwenguni, WHO Dkt. Margaret Chan akihutubia kikao hicho amesema..

(Sauti ya Dkt. Chan)

“Haki ya kupata afya inategemea mamlaka za usimamizi ambazo zinahakikisha maji, hewa na chakula ni salama na vile vile raia wanalindwa dhidi ya kemikali hatarishi ikiwemo uchafuzi wa hewa.”