Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wabunge duniani mbioni kuziba pengo la kutokuwepo usawa:IPU

Wabunge duniani mbioni kuziba pengo la kutokuwepo usawa:IPU

Ukielezea hofu yake ya kutokuwepo kwa usawa wa kisiasa, kijamii na kiuchumi duniani , muungano wa mabunge duniani IPU umetoa wito wa hatua za haraka kubadili mwenendo huo na kutomuacha yeyote nyuma.

Katika azimio lililotolewa Alhamisi wakati wa kufunga mkutano 136 wa baraza kuu la IPU mjini Dhaka Bangladesh, wajumbe wa IPU wameeleza kwamba kutokuwepo usawa kunakuja na gharama kubwa katika jamii , ikiwemo kunadumaza ukuaji wa uchumi, kuaathiri mchakato wa demokrasia na maingiliano ya kijamii na kuongeza hatari ya ghasia na ukosefu wa usalama.

Wabunge hao wamebaini hatua za kuchukuliwa kuhakikisha uchumi unanufaisha wote katika jamii ikiwemo kuimarisha ulinzi wa haki za wafanyakazi ikiwa ni pamoja na haki ya kuishi maisha yenye hadhi na kuboresha ushirikiano wa kimataifa.

Pia wabunge hao wameahidi kushughulikia malengo ya maendeleo endelevu SDG’s hususani lengo namba 10 na kukomesha kutokuwepo usawa ndani na miongoni mwa nchi.

Watu 1206 wamehudhuria mkutano huo wakiwemo wabunge 607 kutoka nchi 126, pia maspika wa bunge 46, manaibu spika 36 na wabunge wanawake 191.