Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uhalifu wa kivita bado unaendelea Syria:Guterres

Uhalifu wa kivita bado unaendelea Syria:Guterres

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amesema ukielekea mwaka wa saba kwa vita vya syia athari za vita hivyo ni kubwa huku ugaidi, uhalifu wa kivita na ukiukwaji mkubwa wa sheria za kimataifa unaendelea. Flora Nducha na taarifa kamili

(TAARIFAYA FLORA)

Natts……

Wakati milio ya mabomu, ….vilio na majonzi vikitawala kila uchao, ikiwemo mauaji ya kutisha ya matumizi ya silaha za kemikali hapo jana Guterres , akizungumza kwenye mkutano wa kimataifa wa usaidizi wa mustakhbali wa Syria mjini Brussels Jumatano amesisitiza kwamba mshikamano wa kimataifa unahitajika kuwasaidia mamilioni ya Wasyria ndani na nje lakini pia katika kuleta suluhu ya kisiasa kwani

(SAUTI YA GUTERRES)

“Hakuna mtu anayeshinda vita hivi, kila mtu anapoteza na inatuweka hatarini sisi sote. Na vita dhidi ya ugaidi ni muhimu , na mafanikio yoyote hayatakuwa na maana bila suluhu ya kisiasa Syraia, uhalifu na ukatili umekuwa.”

Amesema juhudi zimefanyika na msaada umetolewa lakini hautoshi kuichagiza jumuiya ya kimataifa kujitoa kimasomaso kunusuru mamilioni ya watu wanaohitaji msaada sababu

(SAUTI YA GUTERRES CUT 2)

"Uhalifu na ukatili vimekuwa nembo ya vita hivyo, maelfu ya maisha ya watu yamepotea, mamilioni ya familia kutawanywa, na jamii nchini nzima zimesambaratishwa.”

Na kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa New York Baraza la usalama limekuwa na kikao cha dharura kujadili shambulio la linalodaiwa kuwa na silaha za kemikali Syria,kwenye jimbo la Idlib Jumanne. Mwakilishi wa idara ya uponoknyaji silaha ya Umoja wa Mataifa Kim Won soo amesema uchunguzi unaendelea , uwajibikaji utafuata na

(SAUTI YA KIM SOO)

"Endapo itathibitishwa hilo litakuwa shambulio moja kubwa kabisa la matumizi ya silaha za kemikali nchini Syria tangu shambulio la Gutta la August 2013"