Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Waalimu wa shule wasiwajibishwe kwa mipango ya majanga

Waalimu wa shule wasiwajibishwe kwa mipango ya majanga

Walimu wa shule wana majukumu ya kutosha darasani bila kutarajiwa kuwa wsimamizi wa kudhibiti hatari ya majanga pia.

Mtazamo huo ni kwa mujibu wa Jair Torres, mtaalamu wa upunguzaji hatari ya majanga kwnye shirika la Umoja wa Mataifa la elimu, sayansi na utamaduni UNESCO.

Akiwasilisha mkakati wa tano wa UNESCO katika upunguzaji wa hatari ya majanga kwenye mkutano wa kikanda unaofanyika Montreal Canada kuhusu upunguzaji wa majanga kanda ya Amerika, amesema, serikali na mashirika yasiyo ya kiserikali yaani NGO’s wanahitaji kuwapa msaada waalimu katika mfumo wa utaalamu, ikiwa kama sehemu ya kuzifanya shule kuwa salama na zenye kuhimili mikiki ya majanga.