Skip to main content

Tanzania inajitahidi katika vita dhidi ya mihadarati:UM

Tanzania inajitahidi katika vita dhidi ya mihadarati:UM

Umoja wa Mataifa kwa ushirikiano na serikali ya Tanzania jumatatu wamezindua ripoti kuhusu matumizi ya dawa za kulevya iliyotolewa na bodi ya kimataifa ya kuzuia dawa za kulevya INCB kwa mwaka 2016.

Ripoti hiyo imejikita na athari na matumizi ya dawa hizo kwa wanawake,, akiizungumzia mjini Dar Es salaam Tanzania Mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa Bwana Rodriguez Alvaro ameipongeza serikali ya Tanzania kwa kuchukua hatua kubwa kukabiliana na usafirishaji wa dawa za kulevya na matumizi yake , akisema juhudi hizo pia zimesaidia kuielimishja jamii miongoni mwa watanzania kuhusu hatari matumizi ya mihadarati hiyo.

Aameongeza kuwa serikali za Afrika Mashariki zinapaswa kushirikiana na dunia kwa ujumla katika vita dhidi ya dawa za kulevya ingawa utamaduni na sheria zinatofautioana wakati mwingine.

(SAUTI YA ALVARO)

“Ripoti imetolewa kwa ajili ya serikali zote duniani, hata hivyo nchi zina utamaduni na mwenendo tofauti, katika baadhi ya nchi kuna aina Fulani za dawa ni halali , wakati katika baadhi ya nchi zingine ni haramu, mfano Kenya mirungi ni halali kutumia wakati Tanzania matumizi yake ni haramu”