Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tamasha la kibunifu kwa ajili ya SDG's kuanza kesho Bonn

Tamasha la kibunifu kwa ajili ya SDG's kuanza kesho Bonn

Mkutano wa kwanza unaotumia michezo ya kidijitali kuchagiza ufumbuzi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDG's , unaanza kesho huko Bonn, Ujerumani ukitarajiwa kumalizika Ijumaa. Taarifa kamili na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Mkutano huo ujulikanao kama "Tamasha la Kimataifa la Fikra" ni wa aina yake kuwahi kufanyika, na utawaleta pamoja watu 1000 ikijumuisha watunga sera, wanataaluma, asasi za kiraia, makampuni ya kibinafsi, na wataalamu wa michezo ya kidigitali kutoka mataifa 80 ulimwenguni.

Katika chumba kimoja wadau hao watacheza mchezo kama ilivyo katika hali halisi kwa kutumia App, ijulikanayo kama "Hive Mind 2030" , yenye lengo la kufikia malengo ya SDG's.

image
Baadhi ya vioski ambamo kwavyo mkutano huo utafanyika. (Picha:UN/Idhaa ya Kiswahili/Amina Hassan)
Akihojiwa na Redio ya Umoja wa Mataifa, Mitchell Toomey, Mkurungezi wa Kampeni ya Umoja wa Mataifa kuhusu SDG's anasema...

(Sauti ya Mitchell)

"Wazo hili yenye kuvutia, ya kuunda app ya mchezo inayotoa fursa kwa watu kushirikiana katika utekelezaji wa SDGs kwa kutumia nchi bandia, ni jambo la kushangaza sana, kwani unategemea watu kuja pamoja, kuchangia kile wanachokijua, kubadilishana sera na ushauri, kushirikiana, na kuleta mawazo mazuri kwa nguvu ili kupata watu wa kutosha kuwafikiria na kuwaunga mkono kwa wakati mmoja."