Bahari njema kwa kizazi kijacho :Thomson

Bahari njema kwa kizazi kijacho :Thomson

Rais wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa Peter Thomson ametoa wito kwa nchi wanachama kuchukua hatua kupunguza uchafuzi unaoendelea katika bahari.

Bwana Thomson amesema hayo wakati wa mkutano wa siku mbili unaofanyika katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa mjini New York, kuanzia leo Februari 15 hadi 16, kwa ajili ya kufanya maandalizi ya mkutano mkubwa hapo mwezi Juni mwaka huu kujadili lengo 14 la maendeleo endelevu SDGs kwa ajili ya matumizi endelevu ya bahari, maziwa na rasilimali za baharini.

Amesema kuchukua hatua hizo kunaweza kubadilisha hali.

(Sauti ya Thomson)  

Leo tuna nafasi ya kuifanya dunia bora tusirudi nyuma. Tuzingatie msimamo uliotolewa kuleta lengo hili ili kubadilisha hali ilivyo sasa kwenye bahari zetu tuna fursa na tuichukue kuhakikisha tunaitatua kufikia mwaka wa 2030. Juhudi zetu zitaonyesha kama tunaweza kufanya bahari kuwa mahali pema kwa vizazi vijavyo kama vile tulivyoona kwenye ujana wetu tusiwanyime fursa hiyo.

Naye Mkuu wa Idara ya uchumi na kijamii ya Umoja wa Mataifa Wu Hongbo ambaye pia ni Katibu Mkuu wa mkutano huo amesema.

(Sauti ya Wu) 

Sote lazima kujihusisha kutafuta suluhisho popote pale tulipo kama tuna bahari, ziwa kwenye nchi zetu au la. Bahari. Sote tunategemea kwenye bahari na rasilimali za baharini kwa maisha, kwa biashara, maendeleo. Hivyo basi ni muhimu kufikia kila mtu na ujumbe huu.