Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanamhusu kila mtu: Ashe

John William Ashe, Rais wa Baraza kuu la UM.@UNPhoto/Evan Schneider

Magonjwa yasiyo ya kuambukiza yanamhusu kila mtu: Ashe

Rais wa Baraza Kuu, John Ashe, ameongoza leo mjadala maalum kuhushu jinsi ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyo ya kuambukiza, kwa ushirikiano na Shirika la Afya Duniani, WHO, na wasayansi, watafiti na wadau kutoka jamii, sekta binafsi, na mashirika yasiyo ya serikali.

Ashe amesema, magonjwa hayo yanamhusu kila mtu, akiongeza hakuna mmjoa asiyekuwa na ndugu ambaye ameathirika nayo:

“ Kila nyumba, kila jamii duniani kote inajua kuhusu janga hilo, iwe saratani, ugonjwa wa moyo, kisukari au magonjwa ya mapafu”.

Ashe amesema, bado kuna changamoto nyingi, hasa:

““ Mwelekeo wa kufa kwa magonjwa hayo ni asilimia 10 kwenye nchi zilizoendelea, na asilimia 60 kwenye nchi zinazoendelea. Tofauti hiyo kubwa inatukumbusha kwamba suluhu la jumla linaomba ushiriano wa wadau wote”

Amewaomba wadau hao wachukue hatua ili kupunguza idadi ya vifo vinavyosababishwa na magonjwa hayo, akichukua mfano wa kampuni za utengenezaji wa vyakula zilizojitahidi kupunguza sukari na chumvi ndani ya vyakula vya watoto.

Amesisitiza umuhimu wa kulipa kipaumbele suala hilo zima wakati wa kuandaa ajenda ya maendeleo endelevu baada ya 2015.