Kamati ya kupinga unyanyasaji dhidi ya wanawake yaanza kikao cha 66 Geneva.

13 Februari 2017

Kamati ya kuondoa unyanyasaji dhidi ya wanawake CEDAW, hii leo imefungua mkutano wake wa 66 mjini Geneva Uswisi, kamati hiyo imeeleza kuongezeka kwa vitendo hivyo kunakochochewa na wimbi la wakimbizi na wahamiaji duniani.

Orest Nowosad ambaye ni mkuu wa vikundi vya kujikita katika kitengo cha mikataba ya haki za binadamu kwenye ofisi ya Umoja wa Mataifa ya haki za binadamu, ameonya katika hotuba yake ya ufunguzi kuhusu ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake unaongezeka katika mukatdha wa wahamiaji na wakimbizi

Amesisitiza umuhimu wa kuheshimu misingi ya mkataba wa kuondoa aina zote za unyanyasaji dhidi ya wanawake na ushauri wa kamati kwa nchi wanachama .

Pia ameangazia ajenda ya maensdeleo ya 2030 na uhusiano wake na makataba huo ambao umeptishwa na takrigani nchi zote wanachama wa Umoja wa Mataifa, ambapo nchi hizo zina umuhimu katika kutekeleza SDGs na kumarisha uwajibikaji kwa kufanikisha usawa na kuwezesha wanawake na wasichana.

 

♦ Tafadhali iwapo unataka kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud