WFP, Japan wasaidia upatikanaji wa chakula

WFP, Japan wasaidia upatikanaji wa chakula

Shirika la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, limekaribisha mchango wa dola million 85.2 kutoka kwa serikali ya Japani, ambao utasaidia kushughulikia mahitaji ya msingi ya chakula na lishe kwenye nchi 33 katika bara la Afrika, Asia, na ukanda wa Mashariki ya Kati. John Kibego na taarifa kamili

(TAARIFA YA KIBEGO)

ojiro Nakai, Mkuu wa Ofisi ya masuala ya Japani katika WFP, amema mchango huo umepokewa wakati ambapo idadi ya wanaosaka usalama na chakula inaongezeka kwa kasi, na kuipongeza serikali ya Japan kwa kushabikia juhudi za kutambua uhusiano kati ya shughuli za kibinadamu na maendeleo.

Amefafanua kuwa karibu nusu ya fedha hizo itasaidia kuwezesha operesheni za WFP, katika nchi 23 za Afrika ikiwemo Malawi, Lesotho na Swaziland, ambako El Niño imeathiri vibaya uhakika wa chakula kwa mamilioni ya watu.

Asilimia arobaini ya mchango huo wa Japan itasaidia wakimbizi na wakimbizi wa ndani nchini Nigeria, Cameroon Syria, Iraq na Yemen.

Pia utanufaisha WFP, kuimarisha usafiri wake nchini, Sudan, na Sudan Kusini na Afghanistan ambako shirika hilo linasimamia huduma ya anga, usafiri muhimu wa angani na usafirishaji wa mizigo wa Umoja wa Mataifa kwa ajili ya jamii nzima ya kibinadamu.