Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Takriban watu milioni 50 kote duniani wana kifafa: WHO

Takriban watu milioni 50 kote duniani wana kifafa: WHO

Kifafa ni tatizo sugu la ubongo linaloathiri watu kote duniani na linaambatana na tabia ya kujirudioarudia.

Kwa mujibu wa shirika la afya duniani WHO makadiirio ya watu wnaoanguka kifafa kwa wakati mmoja ni kati ya wanne na 10 kwa kila kati ya watu 100.

Tangu mwaka 1997 WHO na washirika wake walizindua kampeni ya kimataifa iitwayo "Out of the Shadows" kwa lengo la kutoa taarifa bora na kuchagiza umma kuhusu tatizo la kifafa.

Takribani watu milioni 50 kote duniani wana kifafa na kufanya tatizo hilo kuwa moja ya magonjwa makuba ya mishipa ya fahamu duniani. WHO inasema karibu asilimia 80 ya watu wenye kifafa wanaishi katika mataifa ya kipato cha chini na cha wastani, huku wengi wa wagonjwa hao na familia zao wakikabiliwa na unyanyapaa na ubaguzi.