Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 748 zasakwa kunusuru binadamu DRC

Dola milioni 748 zasakwa kunusuru binadamu DRC

Mashirika ya kibinadamu pamoja na serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo,, DRC, wamezindua ombi la dola milioni 748 kwa ajili ya kukidhi mahitaji kwa watu milioni 6.7 walioathiriwa na mojawapo ya mizozo mikubwa zaidi kwa muda mrefu katika nchi hiyo.  Maelezo zaidi na John Kibego.

(Taarifa ya John Kibego)

Taarifa ya pamoja ya ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA imesema fedha hizo kwa mwaka 2017 pekee, ni awamu ya kwanza ya msaada unaohitajika kwa ajili ya kutekeleza mpango wa miaka mitatu wa msaada wa kibinadamu nchini humo.

Ombi hilo lililozinduliwa mjini Kinshasa, linalenga miongoni mwa mengine kukidhi mahitaji ya  wakimbizi wa ndani zaidi ya milioni 2.1, watoto zaidi ya 500,000 walio na umri wa chini ya miaka mitano, ambao wanakabiliwa na utapiamlo uliokithiri na maelfu wanaotishiwa na magonjwa ya mlipuko hasa kipindupindu na surua.

Zaidi ya watu nusu milioni walikimbia vurugu mnamo 2016, hasa katika majimbo matatu  ya Kassai, Mkoa wa Tanganyika na kuaachwa katika uhitaji wa msaada msaada kandoni mwa maelfu ya wasudan kusini waliokimbilia Mashariki mwa nchi hiyo.

Rein Paulsen, Mkuu wa ofisi ya uragibishaji wa misaada nchi DRC, amesema ni lazima fedha hizo zitafutwe ili kukidhi mahitaji ya msingi yanayoongezeka miongoni mwa wakimbizi hao.