Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuongeze kasi kutokomeza FGM- UNFPA, UNICEF

Tuongeze kasi kutokomeza FGM- UNFPA, UNICEF

Shirika la mpango wa idadi ya watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA na lile la kuhudumia watoto, UNICEF yamesema dunia lazima iongeze kasi katika kutokomeza ukeketaji watoto wa kike na wanawake, FGM, ifikapo mwaka 2030.

Dkt. Babatunde Osotimehin ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa UNFPA na Anthony Lake wa UNICEF wamesema hayo leo katika taarifa yao ya pamoja ya siku ya kupinga FGM wakisema licha ya kuhatarisha afya ya uzazi ya kundi hilo, mila hiyo potofu huwapokonya mamlaka yao na pia hukiuka haki zao za kibinadamu.

Wamesema pamoja na maendeleo yaliyopatikana kutokomeza bado mamilioni ya wasichana watakeketwa mwaka huu hivyo lazima hatua zichukuliwe kuwalinda.

Bwana Osotimehin na Bwana Lake wamesisitiza umuhimu wa kuweka mazingira ya huduma kwa wale waliokumbwa na FGM na wale walionusurika, bila kusahau kueneza taarifa kuhusu madhara ya kitendo hicho na manufaa ya kutokomeza.

Nchini Kenya Caroline Murgor, mratibu wa taifa wa mradi wa pamoja wa UNICEF na UNFPA dhidi ya ukeketaji anasema uhamasishaji mashinani umeleta nuru akitolea mfano kaunti ya Narok.

(Sauti ya Caroline)