Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Muswada wa ujenzi wa makazi Palestina utazorotesha matumaini ya amani: UM

Muswada wa ujenzi wa makazi Palestina utazorotesha matumaini ya amani: UM

Umoja wa Mataifa umeeleza wasiwasi kwake kuhusu upigaji kura wa muswada wa ujenzi holela wa makazi katika ukingo wa Magharibi ambao umesema utaendeleza matumizi ya ardhi inayomilikiwa na Palestina.

Katika taarifa yake, Mratibu Maalum wa Umoja huo katika mchakato wa amani Mashariki ya Kati, Nickolay Mladenov amesema upitishwaji wa sheria ya ujenzi wa mara kwa mara utadidimiza matumaini ya amani katika ukanda huo.

Muswada huo umeelezwa na kiongozi huyo kuwa una madhara ya kisheria kwa Israel

Mladenov amesema muswada huo ambao umepangwa kupigiwa kura umekuwa ukiwezeshwa kinyume na sheria na mwanasheria mkuu wa Israel na unakiuka sheria za kimataifa.