Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wapiganaji wa zamani wa SPLM/IO waomba kuunganishwa na familia zao

Wapiganaji wa zamani wa SPLM/IO waomba kuunganishwa na familia zao

Wapiganaji wa zamani wa kikundi cha SPLM upande wa upinzani nchini Sudan Kusini waliopatiwa hifadhi huko Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC wameomba usaidizi ili waungane na familia zao wakisema kuwa hawana nia tena ya kurejea kwenye mapigano. Grace Kaneiya ya ripoti kamili.

(Taarifa ya Grace)

Wamesema hayo huko Goma, jimbo la Kivu Kaskazini wakati wa ziara ya mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kwa Maziwa Makuu, Said Djinnit na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, DRC, Maman Samba Sidikou.

Wapiganaji hao wameomba kuunganishwa na familia zao huku wakishukuru ujumbe wa Umoja wa Mataifa, nchini DRC, MONUSCO kwa kuendelea kuwasaidia.

Naye Gavana wa jimbo la Kivu Kaskazini Julien Paluku, amesisitiza umuhimu wa wapiganaji hao kuhamishiwa sehemu nyingine kwa hofu ya kwamba uwepo wao unaweza kusababisha ukosefu wa amani kwenye eneo hilo.

Bwana Djinnit na Bwana Sidikou wameahidi kusaka suluhu kwa ushirikiano na serikali ya DRC, IGAD na Muungano wa Afrika.