Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Makuabaliano ya uchaguzi DRC yazingatiwe-Ladsous

Makuabaliano ya uchaguzi DRC yazingatiwe-Ladsous

Baraza la usalama leo limekutana kujadili hali nchini Jmahuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC wakati huu ambapo Umoja wa Mataifa umemtaka Rais Joseph Kabila wa taifa hilo kuunga mkono hadharani makubaliano ya kisiasa kuhusu uchaguzi huru na wa haki nchini humo. Assumpta Massoi na taarifa  kamili.

(TAARIFA YA ASSUMPTA)

Kikao cha baraza la usalama kinakutana hii leo, huku kukiwa na taarifa za vifo vya takribani watu 100 kufuatia maandamano ya kupinga hatua ya Rais Kabila kuondoka madarakani baada ya kipindi chake cha uongozi

Mkuu wa operesheni za ulinzi wa usalama UM Hervé  Ladsous ameliambia baraza hilo kuwa DRC inapaswa kuchukua hatua kwa kuchunguza matumizi ya nguvu za ziada dhidi ya raia mnamo Disemba 19 na 20 na kwawajibisha wahusika.

Amesema ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO utaendelea kusaidiana na vikosi vya serikali katika kuvinyamazisha vikundi vyenye silaha

Kuhusu uchaguzi Ladous amesema.

( Sauti Ladsous)

‘Tutawajumuisha wajumbe wa baraza la usalama, serikali ya DRC na wadau wengine katika majuma yajayo ili kuzingatia namna ujumbe unavyoweza kuimarisha hali ya kisiasa na kiusalama na kusaidia utekelezaji wa makubaliano ya Disemba 31’’