Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wenyeji na wakimbizi wa ndani Cameroon wanahitaji msaada wa dharura

Wenyeji na wakimbizi wa ndani Cameroon wanahitaji msaada wa dharura

Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa nchini Cameroon ambaye pia ni mratibu wa misaada ya kibinadamu katika ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu OCHA, Najat Rochdi amesema kuwa wenyeji na wakimbizi wa ndani nao pia wanahitaji msaada wa dharura kwani wako hatarini kukumbwa na uhaba wa chakula hususan maeneo ya mpakani mwa Nigeria.

Amesema hayo akihojiwa na Idhaa ya Umoja wa Mataifa wakati huu ambapo hali ya kibinadamu kwenye maeneo hayo inaelezwa kuwa si nzuri.

(Sauti ya Najat) cut1

 “Wenyeji waliokaribisha wakimbizi wa ndani wanajikuta pia kwenye mazingira magumu ambapo wao pia wanalazimika kupunguza kiwango cha chakula wanachokula kwa sikuili kuweza kukidhi pia mahitaji ya wageni wao. Unakuta kaya moja ina watu watano sasa wanalisha watu zaidi ya ishirini na wanane.”