Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA yazindua ombi kukwamua wapalestina

UNRWA yazindua ombi kukwamua wapalestina

Shirika la Umoja wa Mataifa la usaidizi kwa wakimbizi wa Palestina, UNRWA leo limezindua maombi mawili yenye thamani ya dola milioni 813 ili kukidhi mahitaji ya dharura ya wapalestina. Taarifa kamili na Rosemary Musumba.

(Taarifa ya Rosemary)

Dola milioni 402 ni kwa wapalestina walio kwenye maeneo yanayokaliwa na Israel huko Yerusalem Mashariki ilhali dola milioni 411 ni kwa wale walioathiriwa na mzozo wa Syria, wakiwemo wale walioko Lebanon.

Kamishna Mkuu wa UNRWA, Pierre Krähenbühl amesema wakimbizi milioni 1.6 wa Palestina wako kwenye hali mbaya, mahitaji yao yakiongezeka kila uchao hivyo ombi lake ni kwa jumuiya ya kimataifa kuchangia ombi hilo.

(Sauti ya Pierre)

"Hali inayoshuhudiwa Gaza sio ambayo inapuuzwa kwa sababu taarifa hazipo lakini ni moja ambayo madhara yake yamepuuzwa, na haya yote yanafanyika chini ya uangalizi wa jamii ya kimataifa na kwa mtazamo wangu sioni dalili zozote za  kuonyesha kusawazisha maswala ya kijamii, kuichumi kuambatana na utu wa binadamu au usalama kwa ajili ya mtu yeyote katika eneo hilo."