Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Picha mahsusi ya Ban yazinduliwa UM:

Picha mahsusi ya Ban yazinduliwa UM:

Picha mpya ya kuchora ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeondoka Ban Ki-moon imezinduliwa rasmi Jumatano kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa . Mchoraji wa picha hiyo Lee Won-Hee msanii kutoka Korea Kusini amesema “hii ni kazi mahsusi kabisa katika maisha yangu ya usanii”

Lee, amewachora marais na viongozi wengine wakubwa wa kisiasa nchini Korea Kusini , lakini picha ya Katibu Mkuu Ban ndio kazi yake kubwa yenye hadhi ya juu kabisa kuwahi kuifanya

Bwana Lee , amehudhuria uzinduzi wa picha hiyo ambayo sasa imepandishwa ukutani sanjari na picha zingine saba za makatibu wakuu waliotangulia kwenye ukumbi wa mapokezi wa makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Akizungumza kupitia mkalimani Lee amesema uchoraji wa picha hiyo umemchukua takriban miezi sita.

 (SAUTI YA LEE) 

“Niliweza kuja mkwenye Umoja wa mataifa mwezi wa April waka huu na nikapata fursa ya kuzungumza naye , na pia nikampiga picha ofisini kwake na katika mazungumzo yangu na Katibu Mkuu niliweza kubaini wasifu wake na nikajaribu kuutafsiri kwa njia yangu”