Theluthi ya vituo vya afya Borno Nigeria imesambaratishwa: WHO

Theluthi ya vituo vya afya Borno Nigeria imesambaratishwa: WHO

Theluthi moja ya zaidi ya vituo vya afya 700 kwenye jimbo la Borno Kaskazini Mashariki mwa Nigeria vimesambaratishwa kabisa imesema ripoti ya shirika la afya duniani WHO iliyotolewa leo. Pia theluthi ya vituo vilivyosalia havifanyi kazi kabisa.

Ripoti imeongeza kwamba kutokuwepo usalama, ukosefu wa wahudumu wa afya, dawa, vifaa na mahitaji ya lazima kama maji safi, vinafanya fursa za huduma za afya za kuokoa maisha kuwa vigumu kwa watu wa maeneo yaliyoathirika na machafuko ya kundi la Boko Haram. Dr Jorge Castilla ni afisa na meneja wa masuala ya dharura wa WHO kwa Nigeria

(SAUTI DR JORGE)

‘‘Moja ya vitu tulivyoshuhudia pale ni mlipuko wa surua, na kwa kuwa mfumo wa afya uliharibika, hakukuwa na hatua iliyochukuliwa. Kwa sababu hiyo tunaelekeza rasilimali zote za WHO kusaidia kwakuwa hili ni janga kubwa.’’