Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya wakimbizi wa DRC wamiminika Burundi

Mamia ya wakimbizi wa DRC wamiminika Burundi

Kwa zaidi ya juma moja, wakimbizi zaidi ya 200 kutoka Jamuhuri ya Kidemkorasia ya Congo wamevuka mpaka na kuingia Burundi wakikimbia machafuko kati ya majeshi ya serikali na waasi mashariki mwa nchi hiyo katika mkoa wa Kivu ya kusini.

Wakimbizi hao wamepokelewa katika kambi ya muda ya Cishemere magharibi mwa Burundi na kupewa huduma ya kwanza na shirikala Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR na wadau wake.

Mwandishi wetu wa maziwa makuu Ramadhani KIBUGA ametembelea kambi hiyo na kutuandalia taarifa hii.

(TAARIFA YA KIBUGA)