Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Lazima kujumuisha wote kwenye mchakato wa amani Sudan Kusini: Mogae

Lazima kujumuisha wote kwenye mchakato wa amani Sudan Kusini: Mogae

Pande zote kinzani nchini Sudan Kusini zimetakiwa kuhakikisha mchakato wa amani unajumuisha wote. Akifungua mkutano wa wadau mjini Juba Sudan Kusini Jumanne Festus Mogae, mwenyekiti wa kamisheni ya pamoja na ufuatiliaji na tathimini (JMEC) amesisitiza umuhimu wa kujumuisha kila mtu kikamilifu katikia masuala ya kisiasa nchini humo akisema sauti na mchango wa viongozi wa dini, wanawake, wazee, sekta binafsi, asasi za kiraia na vijana haviwezi kupuuzwa.

Ameongeza kuwa kutokuwepo usalama kunaathiri uchumi ambao umezorota tangu kuzuka kwa vita Julai 2016

(SAUTI MOGAE CUT 1)

“Tunazitaka pande zote na hususani serikali ya mpito ya Umoja wa Kitaifa kuonyesha uongozi shupavu na kampeni ya uhakika ya amani. Natoa wito kwa Rais wa Jamhuri ya Sudan Kusini na serikali ya mpito kuchukua msimamo wa ngazi ya juu na uliodhahiri katika kuchagiza amani miongoni mwa jamii na raia wa Sudan kusini”

Na kuhusu machafuko amesema

(SAUTI MOGAE CUT 2)

“Vita vibaya na kutokuwepo usalama kumeongeza zahma ya kibinadamu. Maelfu ya watu wanaendelea kukimbilia ugenini. Na wimbi la wakimbizi wa Sudan Kusini wameigeuza kambi ya Bidibidi nchini Uganda kuwa ya tatu kwa ukubwa duniani”