Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Korea yaongoza mwaka wa pili mfululizo kwa utumiaji wa teknologia ya mawasiliano na habari na mawasiliano

Korea yaongoza mwaka wa pili mfululizo kwa utumiaji wa teknologia ya mawasiliano na habari na mawasiliano

Muungano wa teknolojia ya habari na mawasiliano ITU umesema watu wengi wana fursa ya kupata mtandao wa intaneti lakini wengi hawatumii ipasavyo huduma hiyo. Kwenye ripoti ya kila mwaka kwa jina “Upimaji wa habari kwa jamii”

ITU inasema pia kuwa huduma za intaneti hazitoshelezi na kusisitiza kuwa hakuna sera yakinifu za kuhakikisha watu wananufaika na mtandao huo.

Ripoti hii inatambua umuhimu wa kuwepo kwa habari hizi za kuaminika na bila ya upendeleo za kimataifa zinazoonyesha hali ya maendeleo ya mawasiliano ya teknologia yanayotegemewa na serikali, mashirika ya kimataifa, benki za maendeleo na wachambuzi wa sekta binafsi na wawekezaji kote duniani.

Katibu mkuu wa shirika la mawasiliano duniani, ITU, Houlin Zhao amesema ni muhimu kuzingatia kupunguza kwa ujumla kukosekana kwa usawa wa kijamii na kiuchumi ili watu wengi watumie mitandao. Akiongeza kuwa elimu na mapato ni vigezo kwa mautumizi ya intaneti. Amesema teknologia ya habari na mawasiliano ni muhimu kufikia malengo 17 maendeleo endelevu SDGs, na ripoti hii ina jukumu muhimu katika mchakato huo, na kwama wa bila kipimo na kuripoti, hawawezi kufuatilia maendeleo yanayofanywa na kutambua maeneo ambayo yanahitaji hatua.

Jamhuri ya Korea ndio inayoongoza mwaka huu 2016 ikiwa ni wa pili mfululizo kwa mautumizi ya intaneti. Nchi 10 zilizochukua nafasi ni 2 katika kanda ya Asia-Pasifiki na nchi 7 za Ulaya na 3 visiwa vya Caribbean - St. Kitts na Nevis, Dominica, na Grenada. Nchi zote 175 zilizochunguzwa zimeonyesha kuboresha maadili ya upimaji huo na ukuaji mkubwa katika matutumizi ya simu kimataifa na kuongezeka kwa idadi ya watu, hasa kutoka katika nchi zinazoendelea walionufaika na habari na huduma nyingi zinazotolewa kwa njia ya mtandao.