Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wanawake ulimwenguni wafunguka kuhusu ukatili dhidi yao

Wanawake ulimwenguni wafunguka kuhusu ukatili dhidi yao

Ukatili dhidi ya wanawake ni tatizo sugu, na mizizi yake imo kwenye mila na desturi na hata sera mbovu. Kwa muongo mmoja sasa, Umoja wa Mataifa ikishirikiana na wanaharakati na asasi za kiraia, wanahamasisha serikali na jumuiya za kimataifa kulimulika, kufadhili, na hatimaye kutokomeza ukatili huu.

Makala ifuatayo inakupeleka kwa waathirika wa ukatili huu katika sehemu mbali mbali ulimwenguni. Basi ungana na Joseph Msami.