Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dola milioni 82 zahitajika kushughulikia uhakika wa chakula Madagacar

Dola milioni 82 zahitajika kushughulikia uhakika wa chakula Madagacar

[caption id="attachment_301621" align="aligncenter" width="615"]dailynews230c-16

Wakulima Kusini mwa Madagascar waliokumbwa na miaka mitatu ya ukame wanahitaji msaada wa haraka ili waweze kupanda mazao mara msimu wa upanzi utakapoanza Desemba na Januari, limesema shirika la chakula na kilimo FAO na la mpango wa chakula duniani WFP.

Mashirika hayo yanasema ufadhili zaidi unahitajika ili kushughulikia suala la uhakika wa chakula katika eneo hilo. FAO itaanza kugawa miche na mbegu mwezi ujao ikizilenga familia 170,000 katika wiliya iliyoathirika zaidi ya Kusini mwa nchi hiyo na wakati huohuo familia hizo zitapokea msaada wa chakula au fedha taslim kama sehemu ya mpango wa WFP wa kuwasukuma hadi msimu ujao wa mavuno.

Jumla ya dola milioni 82 zinahitajika na hadi sasa wanapungukiwa dola milioni 50.