Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Boko haramu yawatawanya watu karibu 200,000 Cameroon:IOM

Boko haramu yawatawanya watu karibu 200,000 Cameroon:IOM

Takribani watu laki mbili wametawanywa na kuwa wakimbizi wa ndani nchini Cameroon kwenye jimbo la Far Kaskazini mwa nchi hiyo, kutokana na machafuko ya wanamgambo wa Boko Haram.

Hayo ni kwa mujibu wa takwimu za shirika la kimataifa la uhamiaji IOM likiongeza kwamba kuna wakimbizi wengine zaidi ya elfu 26 ambao hawajaorodheshwa huku 59,000 wakiishi kwenye kambi ya wakimbizi ya Minawao. Leonard Doyle ni msemaji wa IOM.