Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania na hatua za kuhimili mabadiliko ya tabianchi

Tanzania na hatua za kuhimili mabadiliko ya tabianchi

Mkataba wa Paris wa mabadiliko ya tabianchi ukiwa umeanza kutekelezwa, nchi nazo zinahakikisha zinachukua hatua kuhimili madhara ya mabadiliko ya tabianchi. Mathalani nchini Tanzania mabadiliko ya tabianchi yamesababisha kina cha bahari kuongezeka na hata maeneo kuanza kumezwa, mengine mengi yakiwa pia hatarini. Je nini kinafanyika? Assumpta Massoi wa Idhaa hii amezungumza kwa njia ya simu na Waziri wa mazingira, January Makamba aliyeko Marrakesh, Morocco akihudhuria mkutano wa COP22 ambapo anaanza kwa kuelezea hatua ambazo nchi yake inachukua.