Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kiwango cha uelewa wa haki za binadamu chazidi kuongezeka

Kiwango cha uelewa wa haki za binadamu chazidi kuongezeka

Tarehe 10 Disemba ni siku ya kimataifa ya haki za binadamu. Siku hii inaturejeshwa mwaka 1948 tamko la haki za binadamu lilipopitishwa na pia mkutano waVienna, uliohusisha pia kuanzishwa kwa ofisi ya umoja wa Mataifa ya haki za binadamu. Haki zote zinaangaziwa ikiwemo ya kuishi, afya, ajira, kumilikimalina hata kuhakikisha wakazi wa dunia hii wanaishi kwa amani na utulivu. Je uelewa wa siku hii ikoje? Na wananchi wanataka nini? Basi ungana na Tamimu Adamu wa Radio washirika Jogoo FM kutoka Ruvuma Tanzania na mwandishi wetu wa Maziwa Makuu Ramadhani Kibuga kutokaBurundikufahamu kile walichokuandalia siku hii ya leo.