Skip to main content

Uzalishaji wa chakula kupungua Syria-FAO

Uzalishaji wa chakula kupungua Syria-FAO

Hali ya usalama na mabadiliko ya tabianchi ni vyanzo vikubwa vya upungufu wa chakula huko nchini Syria. Hii ni kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa Jumanne na shirika la chakula na kilimo, FAO na shirika la mpango wa chakula duniani WFP

Mpango wa kutathmini mazao na uhakika wa chakula au (CFSAM) umesema baada ya miaka 5 ya vita vya wenyewe kwa wenyewe ni dhahiri kuwa sekta ya kilimo nchini humo imeathirika sana, hivyo kusababisha kupanda kwa bei ya vyakula na mazao.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo inakadiriwa kuwa ekari laki tisa tu za ngano ndizo zilipandwa mwaka jana, ikilinganishwa na ekari milioni 1.5 kabla ya vita. Uzalishaji, wakati huo huo inaonyesha umeporomoka kutoka wastani wa tani milioni 3.4 za ngano kuvunwa kabla ya vita , hadi tani milioni 1.5 mwaka huu ikiwa  upungufu wa  asilimia 55.