Skip to main content

Umoja wa Ulaya timiza ahadi ha kuhamisha wakimbizi kutoka Ugiriki- IFRC

Umoja wa Ulaya timiza ahadi ha kuhamisha wakimbizi kutoka Ugiriki- IFRC

Shirikisho la kimataifa la msalaba mwekundu na hilal nyekundu, IFRC limetoa wito kwa Umoja wa Ulaya na wanachama wake kutimiza ahadi yao ya kuwahamisha haraka wakimbizi wanaotafuta hifadhi chini ya mradi wa Umoja huo wa kuhamisha na kuunganisha wakimbizi na familia zao.

Mkuu wa ofisi ya shirika hilo nchini Ugiriki, Ruben Cano amesema hayo leo katika taarifa iliyotolewa mjini Athens, ikienda sambamba na kuwasili nchini humo kwa Rais Barack Obama wa Marekani.

Bwana Cano amesema wafanyakazi wa IFRC wameshuhudia mazingira ya hali ya duni wanakoishi wakimbizi hao na wana wasiwasi kwa ajili ya hali ya baridi inayokaribia na kuwa muda wa kuboreshwa kwa kambi hizi kukamilika ni mdogo.

Amesisitiza kuwa ni muhimu kwamba Ugiriki iwajibike kutoa awamu ya dharura kwa ufumbuzi endelevu wa muda mrefu akisema shirika hilo linaaamini kwamba watu wanapaswa kusaidiwa na kuhamia nje ya makambi na makazi zaidi ya heshima.

Wakimbizi hawa zaidi ya 60,000 wamekuwa nchini Ugiriki yapata miezi nane na hawana uhakika juu ya maisha yao ya baadaye huku wakigubikwa na matatizo mengi ikiwemo ya kiafya na wanakosa taarifa muhimu.